Lililoanzishwa Jumanne tarehe 10 Septemba na waziri wa Utalii Didier M’Pambia, jukwaa hili linazingatia mada: « Kuelekea marekebisho ya sekta ya utalii ». Kwa siku hii ya pili, waziri Muyaya alikuwa miongoni mwa wazungumzaji kwenye paneli kuhusu kukuza taswira ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na wenzake wa wizara ya Utamaduni, Sanaa na Urithi; Posta, Mawasiliano na Teknolojia ya Kidijitali pamoja na Viwanda, na Biashara Ndogo na za Kati.
« Taswira ya nchi huanza na mtazamo wetu sisi wenyewe kabla ya ule wa wengine. Kupitia utalii, hatupaswi kuwaona tu wageni wanaokuja kutembelea nchi yetu, bali pia sisi wananchi wa ndani, kwani nchi yetu ina ukubwa wa bara zima, » alieleza msemaji wa serikali akiwapa ufafanuzi washiriki kuhusu sera ya mawasiliano ya serikali juu ya utalii wa RDC.
Aliendelea kusema: « Kila Mkongo ana jukumu la kuchangia katika taswira ya nchi. Na taswira hii, haipaswi kufikiriwa kwa maana ya jinsi RDC inavyoonekana kutoka nje, bali jinsi Wakongo wanavyoiona taswira ya nchi yao na jinsi wanavyoshiriki katika kuitangaza. Mkutano huu umetupa nafasi ya kubadilishana mawazo na maoni na wadau kutoka majimbo mbalimbali na wale wanaofanya kazi katika sekta ya utalii ili kuandaa ‘bibiliya’ itakayotuongoza vyema kukabiliana na changamoto ya taswira ya nchi yetu. Tumefurahi kuwa sehemu ya kuchangia katika hili. »
Leonard Sangwa













