Matata Mpoyo Mapon, kiyongozi mukuu wa chama cha upinzani cha Uongozi na Utawala kwa Maendeleo, alilaani marufuku ya mamlaka kwa Moïse Katumbi kukanyaga katika jimbo la Kongo ya Kati.
Kulingana na Waziri Mkuu wa zamani wa DRC, kitendo hiki ni kikwazo kwa uhuru wa Moïse Katumbi ambacho kinaweza kuelezewa kuwa ni kinyume cha katiba na kisichokubalika.
“Nimejifunza hivi punde kwamba Moïse Katumbi, mgombea Urais wa Jamhuri, amepigwa marufuku kwenda Kongo ya kati. Ninaona kizuizi hiki cha uhuru wa Moïse kuwa ni kinyume cha sheria na hakikubaliki. Ukiukaji huu wa haki za binadamu unakumbusha udikteta.” Said Matata Mpoyo kwenye akaunti yake ya twitter.
Ikumbukwe kwamba gavana huyo wa zamani wa katanga kubwa, anafaa kusalia Kongo ya kati Jumatano, Mei 23 kwa ziara yake ya kisiasa.
*Gnk RAMAZANI*