Kinshasa: ufunguzi wa kikao cha bunge cha Machi kinachohusu udhibiti wa bunge na mageuzi ya sheria.
Bunge la Kitaifa na Seneti lilifunguliwa Jumatano hii, Machi 15 huko Kinshasa, kikao cha kawaida cha Machi, kilichojitolea zaidi kwa udhibiti wa bunge na mageuzi ya sheria.
Katika hotuba zao za ufunguzi, za viyongozi wa mabaraza mawili ya Bunge walipitia hali ya nchi katika ngazi za kisiasa, kiusalama, kiuchumi, kijamii na kiutamaduni
Kiyongozi wa Bunge, Christophe Mboso alikashifu kuendelea kwa ukosefu wa usalama jambo ambalo linadhoofisha mchakato wa uchaguzi unaoendelea
Ili kukabiliana na changamoto ya usalama nchini DRC haswa, Christophe Mboso anatangaza mageuzi kadhaa ya kipaumbele, haswa katika sekta ya ulinzi na haki ya kitaifa
Akiendelea na ufunguzi wa kikao cha Machi, Modeste Bahati Lukwebo, Rais wa Seneti alielezea wasiwasi wake kuhusu hali tete ya usalama, kuyumba kwa uchumi lakini pia majanga ya asili
Anasema ana wasiwasi kuhusu kushuka kwa thamani ya sarafu hiyo na anaomba hatua za haraka zichukuliwe. Anasema kuwa kiwango cha sasa cha ubadilishaji sokoni ni zaidi ya kile kilichotolewa katika bajeti ya 2023. Hii inazorotesha hadhi ya kijamii ya watu, kulingana na Modeste Bahati Lukwebo
Gnk RAMAZANI