Siku la 01 mwezi la tatu, mueshimiwa presidenti Katebe Ngoy Michel, la tshumba tsha mukutano wa Mkoa,alipo karibisha ujumbe toka Kinshasa ndani yao wizara mabomu na ma suala la ujamii udjiyo lao ni djuu ya kutambua jamii imeathirika kwa mradi mabomu yenye yupo kwa ndani kampuni kubwa walengwa,ndivyo njo ilipo kuwa kipenge ya ujumbe kwa mueshimiwa Katebe Ngoy Michel,yeye ndiye alitaka kudyuwa mahana la ujiwo la ujumbe ilo dju ya uhakika manufaa ya ujamii kati la wa raïa la haut Katanga.
Kiisha kupokewa kwao ,kiongozi la ujumbe iyo, Dieudonné Kishiku,Aka towa mahana la udjiyo lao akisema, ilipo kuwa muhimo kwanza kutowa salamuni la eshimu kwa prezidente la tshumba la mukutano Mkoa,kiisha ilikuwa lazma kufasiriya kipenge la ujiyo ya ujumbe,tena walipokuwa n’a lazma ya kupokea vigundi enye litakao tumiwa ao kuwa tshaguliwa kusudi wao ndiyo watakapo fanya ongezi la kudyuwa usimamizi la majaliwa la mauzo,itikio ya mueshimiwa Katebe Ngoy ilipokywa njema zaidi kudyuwa tena iko mtshaguliwa la raïa na ametaka kuona maisha nzuri la watoto la jimbo lake.
Kwa iyo, wa naibu la jimbo walikuwa kati lao Mama Hélène Mbedu na bwana Trydon Kalumba nao walipo kuwa na wasiwasi kwa kesi ii walipo kuwa ndani la ongezi iyo dyu ya ku tambuwa neno kuhusu vitendo enye ku gusa ujamii ndani la wa raïa la jimbo haut Katanga.
Ya ku dyuwa, mueshimiwa Katebe Ngoy Michel,ame djitowa na iko ame piganisha kwani wa mama,na wa baba pamoja na vijana la Katanga wawe na maisha la ujamii nzuri .
Julio fundi