Operesheni nzuri kwa Chui wa DRC ambao wamepata ushindi wa pili mfululizo kwenye mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 nchini Morocco, Jumatatu hii, Septemba 9, huko Dar es Salaam.
Timu ya taifa ya Congo ilifanikiwa kushinda (2-0) dhidi ya Ethiopia kwenye uwanja wa Benjamin Mpaka nchini Tanzania, kwa kukosa uwanja uliothibitishwa huko Addis Ababa.
Baada ya kipindi cha kwanza bila bao, DRC iliwashinda Walyas wa Ethiopia kwa mabao ya Théo Bongonda (62′) na Fiston Mayele (76′), dakika chache tu baada ya kuingia uwanjani.
Ushindi huu unawaruhusu Chui kuendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwenye kundi H wakiwa na pointi sita, kabla ya kukutana na Tanzania katika mechi mbili za mfululizo mwezi Oktoba ujao huko Kinshasa na Dar es Salaam.
Leonard Sangwa













