Kiongozi mkuu la kigundi ( fondation du fleuve Congo) bwana Souleymane kahuka alipo funguwa Siku la 26 june 2022 kipande la pakadjuma pa kiwanja onatra kitongoji ya kingabwa, mashindano la mpira ( tournoi du fleuve)
Mashindano aya ili tshangisha pa kipande awamu la mwisho karibu timu mnane (8) la vijana wenye biko na myaka 25 na kushuka kwa sababu ya ku sayidiya vijana wenye ku ishi pembeni ya bahari benye bame tsheza vizuri kabumbu.
» Sababu ya mtshezo uyu siyo Pesa enye vigundi watakayo pata ila kunako wazo la usindikizi kwa vijana uhu wapate kunyanuliwa ndani la kazi ya mpira » alipo sema Mweshimiwa Souleymane kahuka yeye alipo onekanaka mara nyingi pamoja na bwana Samuel Etoo mu tshezadji mku la mpira leo amekuwapo kiongozi ya ( fédération camerounaise de football)
Mutshezo uyu imufunuliwa siku ya 26 june na itako funga mlango lake siku ya 15 julai kati ya unduku na umoja .
Ya kudjuwa pakadjuma ni kipande mkuu ya mtaa kingabwa yame djulikana dyuu ya uguruguru,umbalaka na ma tabiya ingine.
FC carrière pamoja FC Ekogeli walio funuwa na walio kubuwana na vipigo ( penalties)kwa iyo FC Ekogeli ndiyo ilipo wina.
Kigundi la ( fondation du fleuve Congo), ilipo anjiswa mwaka 2019 ni wazo la mwanainchi Souleymane Kahuka,ame sayidiya kupitiya ma njia mingi dyu ya kuleta uwezo kwa vijana lolote kwa mutshezo uyu kigundi la ( fondation du fleuve Congo) amekuwa mu kipande la 8 ya utowadji maendeleo kwa wanainchi.
Yulio Mutoto.