Codeco na vigundi vingine wame leta mawuwaji la raïa pa jimbo la Ituri | G.M. LuboyaI
Ilipo fanyizishwa pa chumba la rtnc uko waziri kusika na vyombo la habari Patrick Muyaya,alipokeya liwali wa jimbo la Ituri pamoja mbele ya wapasha habari,walipo towa swali kuhusu msimamo la serkali kipande la Ituri,kwa swali lake waziri Patrick Muyaya, alipo kumbusha kwa wapasha habari ya kwamba Siku 17 mwezi wa Tano ni siku kuu inchini mzima djuu la eshimu ya kazi la vikosi ya Congo ya kidemokratia, na aki fasiriya liwali Luboya maana kuu ya mkutano na wapasha habari.
Kwa ufunuwo lake, liwali Luboya, ame onesha kwa wapasha habari ya kwamba, mawuwaji enye kufyanika kipande la Ituri,ni kigundi la codeco pamoja na vigunde vingine njo wako wanatenda mawuwaji la raïa,ya kudjuwa tangiya nilipo fika pa jimbo la Ituri leo imekuwa mwaka moja,ali yupo sasa kimia pa ali ya mbele ,na akiongeza tena kuna gundi la Zaïre nao izi Siku wame tomboka, kuhusu hesabu ya vigundi enye kubaka silaha, kunako kigundi la fpic,frpi,codeco,Ndano, kiandenga Maimai, Zaïre, wame lamka kusudi waoneshe na serkali ya kwamba nao biko.
kwa mwisho, ame alika wana inchi wote wadji unge pamoja na vikosi na wawe nyuma ya vikosi kusudi amani irudi ndani ya jimbo la Ituri.